●NIRC yasaini mikataba ya ununuzi mitambo ya kuchimba vidima virefu nchiniI

Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, imesaini mkataba wa ununuzi wa mitambo ya kuchimba visima virefu na kampuni ya utengenezaji mitambo hiyo ya Uturuki iitwayo Acarkardesler, ambapo mitambo hiyo itagharimu Dola za Kimarekani 2,821,028.

Akizungumza wakati ya utiaji saini wa makubaliano hayo Mkurugenzi Mkuu Tume yaa Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Raymond Mndolwa, amesema mitambo hiyo inatarajia kuwasili nchini ndani ya miezi miwili na kisha kuanza kazi.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Raymond Mndolwa (kushoto) akiwa na viongozi wa Kampuni ya Acarkardesler, ya utengenezaji mitambo ya uchimbaji visima virefu kutoka Uturuki mara baada ya utiaji wa saini mkataba wa ununuzi wa mitambo ya kuchimba visima hivyo kati ya Tume na Kampuni hiyo ambapo mitambo hiyo itagharimu Dola za Kimarekani 2,821,028.

Mndolwa amesema lengo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kuhakikisha sekta ya kilimo cha Umwagiliaji inakua nchini na kuchangia ukuaji wa uchumi na Pato la Taifa.

Pia ametia saini mkataba na kampuni ya Garnite Co. Limited kwa ajili ya ununuzi wa mitambo aina nya Support Trucks, inayotumika kubeba vifaa vya uchimbaji visima, ambayo imegharimu thamani ya shilingi bilioni 4,330,600,000; na kwamba mitambo hiyo pia inatarajiwa kuwasili mwezi wa sita mwaka huu

“ Mitambo hiyo itatumika kuchimba visima 67,500 katika halmashauri 184 kwa kipindi cha miaka nane ambapo mradi huo wa visima utakuwa na wanufaika wa moja kwa moja zaidi ya 100,000 hususani vijana na wanawake katika maeneo ya vijijini huku eneo litakalomwagiliwa ni wastani wa ekari 2.5 kwa kila mkulima,”amesema.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa (kushoto) akiwa na viongozi wa Kampuni ya Acarkardesler, ya utengenezaji mitambo ya uchimbaji visima virefu kutoka Uturuki mara baada ya utiaji wa saini mkataba wa ununuzi wa mitambo ya kuchimba visima hivyo kati ya Tume na Kampuni hiyo ambapo mitambo hiyo itagharimu Dola za Kimarekani 2,821,028.

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa mwaka huu wa fedha itachimba visima 1,300 ambapo kati ya hivyo visima 70 vitakavyohudumia mikoa 16 ikiwemo Pwani, Tanga, Mara, Songwe, Singida, Manyara, Dodoma, Lindi, Mtwara, Kigoma, Geita, Morogoro, Simiyu, Ruvuma na Njombe vitachimbwa na wakandarasi na visima vinavyobaki vitachimbwa kupitia mitambo inayonunuliwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Raymond Mndolwa akiwa na mwakilishi wa kampuni ya Garnite Co. Limited mara baada ya utiaji saini kwa ajili ya ununuzi wa mitambo aina ya Support Trucks, inayotumika kubeba vifaa vya uchimbaji visima, ambayo imegharimu thamani ya shilingi bilioni 4,330,600,000. Aidha mitambo hiyo inatarajiwa kuwasili nchi ni mwezi wa sita mwaka huu lengo ni kuongeza tija katika visima vya Umwagiliaji.