Na Lookman Miraji, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Hatua hiyo imefikiwa mara baada ya Waziri wa nchi, ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete kuhudhuria katika mkutano wa kimataifa kuhusu soko la ajira uliofanyika januari 29 mwaka huu mjini Riyadh, Saudi Arabia.

Mkutano huo uliowakutanisha Mawaziri wa Kazi na Ajira kutoka nchi zaidi ya 45 duniani kujadili na kuweka mikakati ya kuongeza kazi za staha kwa Vijana kwa kuzingatia mchango wa sayansi na teknolojia.

Baada ya Mkutano huo, Waziri Ridhiwani Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kazi wa Qatar Dkt. Ali Bin Saeed Bin Samikh ambapo wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika masuala ya sekta ya kazi na ajira ili kuwawezesha watanzania kunufaika na fursa za ajira nchini Qatar .

Vilevile, viongozi wameelekeza timu ya Wataalam inayohusisha pande zote kukutana haraka kutathmini utekelezaji wa hati ya makubaliano kati ya Tanzania na Qatar iliyosainiwa mwaka 2014 Nchini Qatar.