Muunguzi mwenye umri wa miaka 32 alifariki katika mji mkuu wa Uganda, Kampala, kutokana na ugonjwa wa Ebola, Wizara ya Afya ya nchi hiyo ilithibitisha siku ya Alhamisi
Wizara ya Afya ya Uganda imethibitisha Alhamisi mlipuko wa ugonjwa wa Virusi vya Sudan vya Ebola katika mji mkuu, Kampala, baada ya matokeo kutoka maabara tatu za kitaifa.
Mgonjwa wa kwanza, muuguzi mwenye umri wa miaka 32 kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kitaifa ya Mulago, alionesha dalili za homa kabla ya kufariki kutokana na kufeli kwa viungo vingi.
Mamlaka zimesema kuwa hakuna mfanyakazi mwingine wa afya au mgonjwa katika wodi aliyeonyesha dalili za ugonjwa huu.
Mifumo ya majibu ya haraka imeanzishwa, na watu 44 waliokuwa na mawasiliano na muuguzi huyo wamebainishwa na watapewa chanjo.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetenga dola milioni 1 kusaidia na kutuma wataalamu wa afya ya umma kusaidia kukabiliana na mlipuko.
Mkurugenzi wa WHO wa kanda, Matshidiso Moeti, alisisitiza umuhimu wa utaalamu wa Uganda katika kukabiliana na dharura za afya ya umma kuwa muhimu katika kudhibiti mlipuko huu.
Ingawa hakuna chanjo iliyothibitishwa dhidi ya Ebola ya Sudan, chanjo za majaribio kutoka kwenye mlipuko uliopita zipo tayari kutumika baada ya kupata idhini inayohitajika.
Sudan Ebola, iliyogunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1976, inajulikana kusambaa kupitia majimaji ya mwili, ikisababisha dalili kama homa, kutapika, kutokwa na damu, na kuharisha.
Mlipuko katika miji mikubwa ni changamoto kutokana na msongamano wa watu na hatari kubwa ya kuambukizana.