Aliyosema Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko

Mara nyingi husemwa kuwa mustakabali wa dunia ni wa Afrika. Kauli hii inahusishwa na idadi kubwa ya vijana Barani Afrika pamoja na utajiri wa rasilimali zake.

Hata hivyo, naamini mtazamo huu chanya pia ni kielelezo cha uongozi wa maono wa Afrika.

Mzungumzaji wetu anayefuata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ni mfano halisi wa aina hii ya uongozi, tangu siku ya kwanza, amefanya kazi bila kuchoka kuhakikisha tunakidhi mahitaji yetu ya nishati huku tukitimiza matarajio ya watu wetu.

Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Sekta ya Nishati nchini Tanzania, katika kipindi cha uongozi wake, Tanzania imefanikiwa kufikia uwezo wa kutosha wa uzalishaji wa umeme na hata kuwa na ziada kubwa.

Ni katika uongozi wake ambapo kila kijiji nchini Tanzania kimeunganishwa na umeme wa gridi, kupitia juhudi zake, Tanzania imeweza kuunganisha gridi yake ya umeme na nchi nne jirani, na hivi karibuni nchi mbili zaidi zitaunganishwa.

Yeye ndiye aliyeongoza Mpango wa Tanzania wa nishati safi ya kupikia ikiwa ni pamoja na kuanzisha mkakati wa kitaifa wa hiyo nchini Tanzania.

Katika majukwaa ya kimataifa, amekuwa mstari wa mbele katika kusukuma mbele ajenda ya nishati safi ya kupikia, ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa Mpango wa Msaada kwa Wanawake wa Afrika kwenye nishati hiyo wakati wa COP28 huko Dubai, alipokuwa mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa nishati safi ya kupikia uliofanyika Paris, na uongozi wake katika miradi mingine mingi ya kimataifa inayohusiana na nishati.

IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO.