Waafrika wanategemea sana matumizi ya kuni hivyo hatuwezi kupuuza madhara pamoja na gharama kubwa ya kuni na mkaa kwa ajili ya ustawi wa wanawake na wasichana.

Hayo yamebainishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan huku akieleza kuwa watu 950 barani Afrika hawana nishati safi ya kupikia hali inayoharibu kabisa Bara la Afrika.

Rais Samia amebainisha hayo leo katika hotuba yake wakati akihutubia katika Mkutano wa nishati wa wakuu wa nchi za Afrika unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Kukosekana kwa nishati safi ya kupikia kunahusishwa na kuongezeka kwa umasikini,uharibifu wa Mazingira pamoja na kukosekana kwa usawa wa kijinsia” alisema.

Tanzania umeweka mkakati wa matumizi ya mishati safi utakaosaidia kupandisha matumizi ya nishati safi kutoka asilimia 10 kwa sasa kufika asilimia 80 ifikapo mwaka 2034.