Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Akinwumi Adesina, amewasili nchini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, utakaofanyika tarehe 27 hadi 28 Januari 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam Dkt. Adesina amepokelewa na Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Albert Chalamila pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Cosato Chumi kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mkutano wa Wakuu wa Nchi utawakutanisha Wakuu wa Nchi za Afrika na wadau muhimu wa sekta ya nishati ili kujadili mikakati ya kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu kwa maendeleo ya Bara la Afrika.
Mkutano huo inatarajiwa kuwa utahudhuriwa na Wakuu wa Nchi 25 na Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu na Naibu Mawaziri Wakuu 10 inafanya idadi ya viongozi wa ngazi ya juu kuwa 35
Wakuu wa Nchi za Algeria, Comoro, Liberia, Lesotho, Botswana, Kenya, Ghana, Gabon, Sierra Leone, Ethiopia, Sudan, Malawi, Zambia, Somalia, Guine Bisau, Burundi, Mauritania, Kongo Brazzaville, Madagascar, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Libya, Nigeria, Djibouti na Gabon watakuwepo nchini kwa ajili ya mkutano huo.
Makamu wa Rais kutoka nchi za Gambia na Benin na Mawaziri Wakuu wa Cote d’Ivoire, Uganda, São Tomé and Príncipe na Equatorial Guinea na Naibu Mawaziri Wakuu ni kutoka nchi za Eswatini na Namibia pia watahudhuria.