Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio awasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ili kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati.


Rais huyo wa Sierra Leone amepokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Kombo pamoja na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila.

Rais Bio ndiye Rais wa Kwanza kuwasili kati ya marais walioalikwa wanaotarajiwa kuwasili siku ya kesho na kesho kutwa kabla ya kuanza kwa Mkutano huo utakaoanza Januari 27 na 28 mwaka huu.


Mkutano huo utakaofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere.