Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, ameendelea kuthibitisha uungaji mkono thabiti kwa Israel, siku chache baada ya kusitishwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza.
Rubio alizungumza na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na kumuhakikishia kwamba Marekani itaendelea kuiunga mkono Israel, hasa wakati huu wa operesheni kubwa ya kijeshi katika mji wa Jenin, Ukingo wa Magharibi. SOMA: Biden: Marekani inasimama na Israel
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Tammy Bruce, alithibitisha kuwa Rubio alizungumza na Netanyahu kupitia simu kutoka Washington jana usiku, akisisitiza kwamba uungaji mkono wa Marekani kwa Israel ni kipaumbele cha Rais Donald Trump.
Aidha, Rubio alimmpongeza Waziri Mkuu Netanyahu kwa mafanikio ya Israel dhidi ya makundi ya Hamas na Hezbollah, na kumuomba kuendelea na juhudi za kuwarejesha mateka wote waliobaki katika ukanda wa Gaza.