KIONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu amempongeza Tundu Lissu kwa kushinda nafasi ya uenyekiti wa Chadema baada kumshinda mstaafu Freeman Mbowe.
Tundu Lissu amepata ushindi wa kura 513 sawa na asilimia 51.5 Odero Charles Odero amepata kura 1 sawa na asilimia 0.1 Freeman Mbowe amepata kura 482 sawa na asiliima 48.3.
“Nakupongeza Ndugu Tundu Lissu kwa kushinda uchaguzi na kuwa mwenyekiti wa chama chako cha Chadema. Kuchaguliwa kwako kunakufanya pia uwe Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania ,” ameandika Kiongozi wa ACT-Wazalendo Dorothy Semu.
“Nikiwa Kiongozi wa ACT Wazalendo nakuhakikishia ushirikiano wa dhati katika kupigania demokrasia ya nchi yetu.,”
“Pia nakupongeza ndugu Freeman Mbowe kukamilisha uongozi na kuachia demokrasia ichukue mkondo wake ndani ya chama chako,” ameandika Kiongozi wa ACT-Wazalendo Dorothy Semu.