Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imetoa wito kwa wananchi kuchukua vitambulisho vyao baada ya kupokea ujumbe mfupi wa simu.

Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji, amesema mamlaka  imefanya maboresho makubwa katika mchakato wa upatikanaji wa vitambulisho ili kurahisisha huduma kwa wananchi.

Amesema lengo la NIDA ni kutoa ufafanuzi kuhusu zoezi linaloendelea la kukusanya vitambulisho vyote vilivyokaa muda mrefu katika ofisi za vijiji, mitaa na kata bila kuchukuliwa na wahusika.

“Kutokana na changamoto hiyo, NIDA ililazimika kukusanya vitambulisho na kuvirejesha katika ofisi za usajili za wilaya nchini kote, kisha kuwatumia wananchi ujumbe mfupi wa simu kuwajulisha kuchukua vitambulisho vyao.

Kwa muda mrefu, kulikuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu kutokupata vitambulisho vyao vya taifa, licha ya kuwa na namba za utambulisho wa taifa (NIN).

Tatizo hili lilichangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa kadighafi za kutosha, tunamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha kiasi cha bilioni 42.5, zilizotuwezesha kununua kadi ghafi 13,738,735, ambazo zimesaidia kuzalisha vitambulisho vya wananchi wote waliokwisha kusajiliwa na kupata namba,” amesema.

Amesema kuanzia Septemba 2023, NIDA ilianza uzalishaji mkubwa wa vitambulisho vya taifa, ikiwa ni pamoja na usambazaji na ugawaji wa vitambulisho kwa wananchi kupitia ofisi za kata, vijiji, na mitaa,Vitongoji na Shehia kwa upande wa Zanzibar.

Uamuzi wa kupeleka vitambulisho katika ofisi za vijiji, kata, na vitongoji ulifanyika kwa nia ya kuwaondolea usumbufu wananchi wa kuvifuata katika ofisi za NIDA za wilaya, na badala yake wavichukue katika ofisi za serikali za mitaa na vijiji wanapoishi.

Vitambulisho vilisambazwa sambamba na orodha ya majina ya wenye vitambulisho na kubandikwa,baada ya hapo tutawatumia wananchi ujumbe mfupi wa simu, ukiwataka wafike katika ofisi za NIDA za wilaya walikojisajili ili kuchukua vitambulisho vyao ndani ya muda ulioelekezwa kwenye ujumbe huo.

Kaji amesema kuhusu kusitishiwa huduma , kama mwananchi atapokea ujumbe mfupi wa simu akatakiwa kuchukua kitambulisho chake  ambavyo havijachukuliwa na asipofika kuchukua  ndani ya muda huo, matumizi ya namba yake ya utambulisho wa taifa yatasitishwa.

“Dhamira yetu na Serikali kwa ujumla ni kuhakikisha, kila kitambulisho kilichotengenezwa kinachukuliwa na mhusika, hasa ikizingatiwa kuwa vimeigharimu pesa nyingi katika utengenezaji wao.Amesema

 Aidha, amewashukuru wananchi wanao endelea kujitokeza sehemu mbalimbali nchini kufuatilia vitambulisho vyao mara tu baada ya kupokea ujumbe mfupi wa simu.

“Wananchi wanatakiwa kuwa wavumilivu, kwani ambaye hajachukua kitambulisho na amejiandikisha namba ya simu atatumiwa ujumbe.

Ni muhimu kueleweka kwamba maelekezo ya kusitisha matumizi ya NIDA yatakuwa kwa wale ambao wametumiwa ujumbe  kupitia simu zao za mkononi, kisha wakaacha kujitokeza kuchukua vitambulisho vyao.

Hata hivyo, kama hukupata ujumbe wa simu unao kujulisha kwamba kitambulisho chako kipo ofisi za NIDA wilaya fulani, namba yako haitazuiliwa.

Kuhusu changamoto ya kuhama eneo kwa baadhi ya wananchi ,ambao wakati wa usajili walikuwa katika maeneo tofauti na wanapoishi sasa, wataweza kuchukua vitambulisho vyao huko waliko.

Tumeruhusu mtu kuchukua kitambulisho cha ndugu au jamaa yake, kwa sharti kwamba mtu anayekwenda kuchukua kitambulisho aende akiwa na ujumbe tulioutuma kwa mwenye kitambulisho pamoja na namba ya NIDA.

Hivyo, kusiwe na kisingizio chochote kuhusu mtu kutokuwepo katika eneo lake la awali ambapo kitambulisho chake kilikuwa kimepelekwa; anaweza sasa kumtuma mtu mwingine kwenda kumchukulia”amesema

Kuhusu suala la baadhi ya vitambulisho kufutika,amesema  Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani alitoa ufafanuzi kwamba itabidi kuchapisha vitambulisho upya kwa wale wote ambao vitambulisho vyao vimefutika bila malipo yoyote.

Tunawatangazia wananchi wote wenye vitambulisho vyenye changamoto kuvirudisha katika ofisi za NIDA za wilaya au katika ofisi za kata, vijiji na mitaa ambapo vilikuw