MKUU wa jeshi la Israel Meja jenerali Herzi Halevi amejiuzulu, kutokana na kushindwa kuzuia uvamizi wa kundi la wanamgambo la Kipalestina la Hamas uliofanyika Oktoba 7 mwaka 2023.

Katika barua yake ya kujiuzulu Halevi amesema sababu kubwa iliyomfanya kujiuzulu  kushindwa kutimiza wajibu wake wa kuzuia uvamizi  huo.

Hatahivyo, amesema anafarijika kuona jeshi la Israel limeweza kupata mafanikio makubwa wakati wa uongozi wake .

Huku kiongozi wa upinzani wa Israek Yair Lapid ameitaka serikali ya waziri mkuu Benjamin Netanyau ijiuzulu baada ya Halevi kujiuzulu.

Wakati huohuo Israel imeanzisha operesheni kubwa ya kijeshi katika mji unaokaliwa kwa mabavu na nchi hiyo wa Jenin,katika Ukingo wa Magharibi na kusababisha vifo vya watu sita na wengine eza maisha na wengine  35 kujeruhiwa.