Na Isri Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Wakili Deogratius Mahinyila mechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema ( BAVICHA ) Taifa, leo Januari 14, 2025.

Mahinyila ametangazwa katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya zoezi la uchaguzi wa viongozi wa baraza hilo kukamilika ambapo amepata kura 214, akimshinda Hamis Masoud aliyepata kura 112.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara ameshinda Necto Kitiga, huku Zanzibar akishinda Abdallah Haji kwa asilimia 91.

Uchaguzi huo umehusisha pia nafasi mbalimbali ikiwemo wajumbe watano wa mkutano mkuu, huku mmoja kati yao akitokea visiwani Zanzibar.

Aidha baraza limechagua qajumbe watano wa Baraza Kuu, ambapo Atfat Ally (Zanzibar) ameongoza kwa kupata kura nyingi kwa asilimia 91, akifuatiwa na Sabitina Makweta, Ester Nyoboriri, Barnaba Samwel na Joel Msuya.