SERIKALI inatarajia kuanza kufanya usaili wa kujaza nafasi 14,648 kwa kada ya walimu kwa shule za msingi na sekondari unaolenga kupunguza uhaba nchini.
Aidha, Rais Samia Suluhu Hassan ametoa vibali vya ajira 155,008 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) 2022-2025. Haya yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene.
Alisema kuanzia Januari 14 hadi Februari 24, mwaka huu serikali itaanza kufanya usaili wa kada za ualimu na kusisitiza kuwa mchakato huo ni shirikishi.
Alisema usaili huo utaendeshwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais (Utumishi), Ofisi ya Rais-Tamisemi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Afya, Tume ya Utumishi wa Walimu, ofisi za wakuu wa mikoa yote na wataalamu kutoka katika taasisi za umma.
Simbachawene alisema usaili huo una lengo la kujaza nafasi 14,648 zilizotolewa na Rais Samia kwa lengo la ku punguza uhaba wa walimu nchini.
“Nafasi zinazoshindaniwa ni za walimu wa shule za msingi na sekondari 14,648 wakati walioomba ni 201,707 unaweza kuona maombi ni mengi nafasi ni chache,” alisema.
Alisema kulingana na mahitaji ya elimu kwa sasa, serikali itaajiri wataalamu wa fani za amali. Alisema usaili wa kada za ualimu utafanyika katika mkoa ambao kila msailiwa anaishi au aliombea kazi na kusisitiza kuwa utaratibu huo umelenga kuwapungu zia gharama za kusafiri na mambo mengine.
“Hivyo nawasihi sana waombaji wote kuhakikisha kila mmoja anakwenda katika kituo ambacho amepangi wa kwa ajili ya usaili kwani mahitaji yake ya msingi yapo huko,” alieleza.
Alisema usaili wa awali wa kuandika (mchujo) kwa kada za ualimu utafanyika kwa njia ya kuandika kwa mkono kwa kada zote na ngazi zote za elimu.
“Ninapenda kuwakum busha wale wote wataka okwenda kwenye usaili wahakikishe wanabeba vyeti vyao halisi kikiwemo cheti cha taaluma na cheti cha ku zaliwa.
Pia, wanapaswa kuja na namba zao za usaili walizotumiwa kwenye akaunti zao za ajira portal pamoja na kuzingatia ratiba kama ilivyopangwa na Sekretarieti ya Ajira.
Alisema pia, wasailiwa wanapaswa kuwa na kit ambulisho halisi kwa ajili ya utambuzi, ikiwa ni pamoja na Kitambulisho cha Taifa (NIDA), hati ya kusafiria, leseni ya udereva, kitambulisho cha mpiga kura, mkaazi, cha kazi au barua ya utambulisho kutoka ofisi ya serikali ya mtaa au shehia anayoishi.
Aidha, Simbachawene alisema Rais Samia ametoa vibali vya ajira 155,008 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapin duzi (CCM) 2022-2025.
Hivi karibuni, Sekretarieti ya Ajira iliendesha mchakato wa kuajiri watumishi wa kada za wataalamu wa afya ambao watumishi 11,483 waliofaulu usaili na wenye sifa stahiki walipangiwa vituo vya kazi katika taasisi za serikali, hatua ambayo imepunguza uhaba mkubwa wa watumishi uliokuwa unaikabili sekta ya afya.