Moto wa nyika ambao umekuwa vigumu kudhibitiwa unateketeza sehemu za Los Angeles, na kusababisha vifo vya takriban watu watano, kuharibu mamia ya majumba, na kulazimisha zaidi ya watu 130,000 kukimbia kutoka majumbani mwao katika jiji la pili kwa ukubwa Marekani.
Licha ya jitihada za wazima moto, miale mikubwa ya moto inaendelea kushika kasi, huku hali ya hewa na athari za mabadiliko ya tabianchi zikitarajiwa kuendelea kuzidisha moto siku zijazo.
Ni yapi yaliojiri?
Zaidi ya watu 137,000 wamekimbia majumbani mwao, wengi wao wakiwa na mizigo kidogo walichoweza kubeba.
Polisi wamesema kuwa watu watano wamepoteza maisha, na miili yao kupatikana karibu na moto wa Eaton, ingawa chanzo cha vifo vyao hakijajulikana. Kama moto wa Palisades ulivyokuwa mkubwa zaidi, moto wa Eaton pia haujaweza kudhibitiwa.
Kwa upande mwingine, moto wa Sunset ambao ulikuwa ukiathiri eneo maarufu la Hollywood Hills umeanza kupungua lakini bado haujadhibitiwa. Amri za uhamishaji kwa eneo la Hollywood Hills West zimeondolewa.
Majumba karibu 2,000 yanajulikana kuharibiwa, ikiwemo nyumba, shule, na biashara katika Barabara maarufu ya Sunset Boulevard. Mtaalamu wa moto, ambaye alizungumza na BBC, alisema kuwa “mitaa yote… imeharibiwa kabisa”.
Miongoni mwa watu maarufu waliopoteza nyumba zao ni Leighton Meester na Adam Brody, walioshiriki tu tuzo za Golden Globe siku chache zilizopita, pamoja na Paris Hilton.
Sekta ya bima inahofia kuwa huu unaweza kuwa mmoja wa milipuko mikubwa ya moto katika historia ya Marekani, na hasara za bima zinatarajiwa kuwa zaidi ya dola bilioni 8 (pesa za Uingereza £6.5 bilioni) kutokana na thamani kubwa ya mali kuteketezwa na moto huo wa nyika.
Hata hivyo, kuna tumaini kidogo kwa wazima moto, kwani hali ya hewa ya moto katika kusini mwa California imeshushwa kutoka “yenye hatari sana” hadi “yenye hatari”.
Lakini mtaalamu wa hali ya hewa wa BBC, Sarah Keith-Lucas, anasema hakuna mvua inayotarajiwa katika eneo hilo kwa angalau wiki moja ijayo, hivyo hali inabakia kuwa huenda moto ukaendelea.
Mafuta ya umeme yamekatwa katika maeneo mengi ya jiji, na msongamano wa magari umeongezeka.
Kwa kuongeza, baadhi ya shule na Chuo Kikuu cha California, Los Angeles (UCLA) vimefungwa.
Mzozo wa kisiasa kuhusu ufanisi wa maandalizi ya jiji wakati wa dharura umeibuka baada ya kugundulika kuwa mabomba ya baadhi ya wazima moto hayakuwa na maji, jambo ambalo limeibuliwa na rais mteule wa Marekani, Donald Trump.
Lakini katika nchi jirani ya Pasadena, Mkuu wa Zimamoto Chad Augustin alisema eneo hilo lilichelewa kidogo kwa uokozi kutokana na maji ya kuzima moto kukosa shinikizo la kurusha maji maghorofani.Lakini Masuala yote yametatuliwa, alisema.
Alihusisha suala hilo na vyombo vingi vya moto kuvuta maji kwa wakati mmoja pamoja na kupoteza kwa shinikizo la kupunguza nguvu ya kurusha maji ya kuzima moto.