Mahakama ya Juu nchini Marekani imetupilia mbali ombi la Rais mteule Donald Trump la kusitisha hukumu dhidi yake hii leo Ijumaa katika kesi inayomkabili ya uhujumu uchumi

Trump alipatikana na hatia ya kughushi nyaraka kwa lengo la kuficha kiwango halisi cha malipo ya kiasi cha dola laki 130 kwa muigizaji wa filamu za ngono Stormy mnamo Daniels kama gharama za kisheria mnao mwaka 2016.

Jaji Juan Merchan, anayesimamia kesi hiyo, ameonyesha kuwa hatofikiria kifungo kwa Trump. Majaji wawili wa kihafidhina walijiunga na watatu wa kisoshalisti kumkataa Trump.

Mahakama tatu za New York pia zilikuwa zimekataa ombi ya kuchelewesha hukumu, na Mahakama ya Juu imetangaza hukumu itafanyika kama ilivyopangwa leo tarehe 10 mwezi Januari 2025 siku chache kabla ya Trump kuapishwa tena kuwa rais.

Baada ya jaji kutoa hukumu ya hatia dhidi ya Trump mwezi Mei 2024, Trump alikubaliana kuwa atahukumiwa Julai, lakini mawakili wake walifanikiwa kumshawishi Jaji Merchan kuchelewesha hukumu mara tatu tofauti.

Trump alijaribu kuomba kinga ya rais mteule dhidi ya mashtaka, lakini waendesha mashtaka wa Manhattan walikataa, wakisisitiza kuwa mashtaka yanapaswa kuendelea.

Hii ni baada ya kumshinda Trump katika mashtaka ya kuingilia uchaguzi wa 2020. Katika kikwazo kingine cha kisheria kwa Trump Alhamisi, Mahakama ya Rufaa ya Shirikisho huko Georgia ilikataa ombi la kuzuia kutolewa kwa sehemu ya ripoti ya mshauri maalum Jack Smith kuhusu njama ya Trump kudhoofisha uhamisho wa madaraka kwa Joe Biden baada ya uchaguzi wa 2020.

Mawakili wa Walt Nauta, msaidizi wa zamani, na Carlos de Oliveira, meneja wa mali wa Mar-a-Lago, walisisitiza kuwa kutolewa kwa ripoti hiyo kungelazimisha kesi za jinai dhidi yao katika siku zijazo.