Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limethibitisha kumshikilia Dkt. Wilbroad Silaa baada ya kumkamata usiku wa kuamkia leo Januari 10, 2024.

Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, SACP Jumanne Murilo amethibitisha leo Januari 10, 2025

“Daktari yupo tuko nae na tumekuwa na mahojiano naye kwa baadhi ya mambo na mahojiano yetu na yeye yanakwenda vizuri”

”Kwa hiyo tunaiangalia mifumo ya kisheria inatuambia nini cha kufanya na taarifa zaidi zitatolewa baadae” amesema Muliro.