Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila ameagiza kuwa ifikapo Januari 20 bajaji na bodaboda hazitaruhusiwa kufika mjini na maeneo yote ya katikati ya mji.
Mkuu wa Mkoa ametoa maagizo yake leo January 9, 2025 jijini Dar es Salaam alipokuwa katika ziara yake ya kukagua ukarabati wa maeneo mbalimbali ya jiji Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa bajaji na bodaboda hazitaruhusiwa kufika katika maeneo yote yaliyoko katikati ya mji ikiwemo Posta na stesheni ili kupunguza msongamano wa vyombo vya moto.
”Ifikapo Januari 20 bajaji na bodaboda hazitaruhusiwa kupita barabara inayoelekea stesheni, barabara inayoelekea katika hoteli ya Johari Rotana pamoja na Hyatt Regency ili kupunguza msongamano barabarani” alisema Chalamila.