Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton amelazwa hospitalini baada ya kupata homa, kwa mujibu wa msemaji wa chama cha Democrat.
“Anasalia katika hali nzuri na anathamini sana utunzaji bora anaopokea,” Angel Ureña aliandika kwenye X, iliyokuwa Twitter.
Alisema Clinton alilazwa katika Kituo cha Matibabu cha Chuo Kikuu cha Georgetown huko Washington, DC siku ya Jumatatu jioni kwa ajili ya vipimo na uchunguzi baada ya kupata homa hiyo.
Taarifa ya Bw Ureña haikutoa maelezo zaidi kuhusu hali ya mwanachama huyo wa demokrat kutoka Arkansas, ingawa ripoti za vyombo vya habari vya Marekani zinaonyesha Clinton anatarajiwa kupata nafuu.