Benki Kuu ya Tanzania inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhamasisha matumizi ya malipo ya kidijitali nchini. Mojawapo ya hatua hizo ni kuhakikisha kuwa malipo yanayofanywa kwa kutumia mashine za malipo za wafanyabiashara (Point of Sale – POS) ni bure kabisa kwa watumiaji wa kadi.
Hivyo, Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuwakumbusha wananchi kwamba malipo yanayofanywa kwa kutumia kadi za benki (debit, credit, au prepaid) kwenye mashine yoyote ya POS hayatozwi ada yoyote. Wafanyabiashara wote wamekatazwa kutoza ada au gharama za ziada kwa miamala inayofanywa kwa mashine za POS.
Benki Kuu inawahimiza Watanzania kuendelea kutumia mifumo ya malipo ya kidijitali, kwa kuwa ni njia salama, rahisi na yenye gharama nafuu ya kukamilisha miamala. Matumizi ya mifumo ya kidijitali, ikiwemo kadi za malipo, huchangia kujenga uchumi wenye matumizi kidogo ya pesa taslimu, na pia huleta faida kama usalama, uwazi na urahisi wa matumizi.
Iwapo mlipaji utatakiwa kulipa ada au gharama za ziada unapotumia mashine yoyote ya POS, tafadhali toa taarifa kwa benki yako au wasiliana na Dawati la Malalamiko la Wateja wa Benki Kuu ya Tanzania kupitia: