Shirika la kukabiliana na majanga nchini Msumbiji limesema kuwa mpaka sasa  idadi ya vifo vilivyotokana na kimbunga Chido vimefikia 94.

Wiki moja sasa tangu Kimbunga Chido kutokea na kuishambulia pwani ya Msumbiji na kuathiri maeneo mengi ikiwemo visiwa vya Mayotte.

Taarifa zinasema kuwa kimbunga hicho  pia kimefanya uharibifu mkubwa katika jimbo la kaskazini la Cabo Delgado.

Takriban watu 620,00 wameathirika na kimbunga hicho nchini Msumbiji, wakati 500,000 kati ya hao wakiishi Cabo Delgado.

Wataalamu wanasema kimbunga Chido kimekuwa na nguvu zaidi kutokana na athari ya mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na shughuli za kibinadamu.

Jimbo la Cabo Delgado hukumbwa mara kwa mara na vimbunga vya tropiki lakini pia jimbo hilo linakabiliwa na vurugu zinazotokana na uasi wa muda mrefu.