Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico amefanya ziara ya kushtukiza mjini Moscow kwa mazungumzo na Vladimir Putin – akiwa ni kiongozi wa tatu pekee wa nchi za Magharibi kukutana na kiongozi huyo wa Urusi tangu uvamizi kamili wa Ukraine miaka mitatu iliyopita.

Fico – mkosoaji mkubwa wa uungaji mkono wa Umoja wa Ulaya kwa Kyiv katika vita – alisema walijadili usambazaji wa gesi ya Urusi kwa Slovakia – ambayo nchi yake inaitegemea.

Mkataba na kampuni kubwa ya gesi ya Gazprom ya kusafirisha nishati kupitia Ukraine hadi Slovakia unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu.

“Maafisa wakuu wa EU walifahamishwa kuhusu safari yangu na madhumuni yake… siku ya Ijumaa,” Fico aliandika kwenye Facebook.