Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesambaza vikosi vya jeshi hilo mitaani kuhakikisha usalama wa raia hasa kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

Sambamba na hilo, jeshi hilo limepiga marufuku watu wasiokuwa na vibali kupiga baruti na fataki katika kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari, akisisitiza kuimarika kwa hali ya ulinzi na usalama katika maeneo mbalimbali, zikiwemo nyumba za ibada ili watu waweze kushiriki ibada zilizoandaliwa katika sikukuu hizo.

Muliro alisema vikosi vyote vya jeshi la polisi viko mitaani kuhakikisha usalama wa raia katika maeneo yote ya Coco beach, Coco Mihogo, Coco Plaza, Sea Cliff, Tegeta, Kunduchi, Kitunda, Mwanagati, Msongola, Kivule, Pugu Kirumba, Pugu kichangani, Pugu mnadani, Pugu Sekondari, maeneo yote ya Kigamboni, Kimara, Bonyokwa na Kwembe kwa Kolimba.

“Maeneo yote hayo tutahakikisha yapo salama na mtu yeyote atakayejihusisha na vitendo vya uhalifu jeshi la polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam halina huruma na mtu anayeitwa mhalifu, tutashughulikia vikali lakini kwa mujibu wa sheria,” alisema Muliro.

Alitoa onyo kwa watu kupiga baruti au fataki bila kuwa na vibali maalumu kwa mujibu wa sheria kwani kuna watu wanapiga baruti katika maeneo yasiyoruhusiwa, hivyo alisema jeshi la polisi linatoa vibali ya kufanya shughuli hizo baada ya kujiridhisha kuwa fataki na baruti hizo zinapigwa wapi na zinasimamiwa na nani.

Alisema polisi inatoa wito kwa watu wanaoendesha vyombo vya moto kufuata sheria za usalama barabarani kwani hawatokuwa na uvumilivu na mtu yeyote atakayefanya vitendo vitakavyosababisha kutendeka kwa makosa.

Pia, aliwaonya madereva kutoendesha vyombo vya moto wakiwa wamelewa, hali inayoweza kusababisha ajali na kuleta madhara makubwa kwa binadamu.

Muliro alisema polisi haitasita kuchukua hatua kali na za haraka za kisheria kuhusiana na watu watakaofanya vitendo vya hovyo na kihalifu chini ya mwamvuli wa kusheherekea sikukuu.

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesambaza vikosi vya jeshi hilo mitaani kuhakikisha usalama wa raia hasa kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

Sambamba na hilo, jeshi hilo limepiga marufuku watu wasiokuwa na vibali kupiga baruti na fataki katika kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari, akisisitiza kuimarika kwa hali ya ulinzi na usalama katika maeneo mbalimbali, zikiwemo nyumba za ibada ili watu waweze kushiriki ibada zilizoandaliwa katika sikukuu hizo.

Advertisement