Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanal Evans Mtambi amewataka viongozi katika mkoa huo kuacha kufanya kazi kwa mazoea wakati wakuwahudunia wananchi nakutokuwa kikwazo cha kutanzua changamoto zinazowakabili
Kanali Mtambi ametoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo kwa kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara ya Uraia na Utawala Bora ambapo amesema mafunzo hayo yakawe sehemu ya kuwasaidia viongozi katika kusaidia kutatua changamoto za wananchi katika maeneo hayo.
“Niwaombe Wizara ya Katiba na Sheria mafunzo haya yawe endelevu muendele kuja kutukumbusha kwa sababu nikawaida ya Binadamu kufanya kazi kwa weredi kuna wakati inafika ule ubinadam, badala ya kufanya kazi kwa weredi tunaanza kufanya kwa mazoea nahapo ndipo tunakinzana na misingi tuliyokumbushwa.
Mtambia amewataka viongozi kwenda kuwa suluhu ya changamoto ya matatizo yanayoikabili jamii kwenye maeneo wanayoyasimamia na kuhakikisha kutokuwa sehemu ya kikwazo ya kutanzua changamoto zinazoikabili jamii.