Mazungumzo yaliyopangwa kufanyika Jumapili ya viongozi wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kumaliza mzozo wa Mashariki mwa Congo yamefutwa baada ya majadiliano kukwama.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mpatanishi wa Umoja wa Afrika kwa ajili ya kumaliza mzozo huo Joan Lourenco, amesema mazungumzo hayo yameshindwa kufanyika kutokana na Rwanda kugoma kushiriki mazungumzo hayo.
Taarifa hiyo pia imeeleza wazi kuwa Rwanda imeitaka Congo ifanye mazungumzo ya moja kwa moja na waasi wa M23 wanaodhibiti eneo kubwa la Mashariki mwa Congo tangu mwaka 2021.
Lourenco amesema kuwa walikuwa na matarajio makubwa na mkutano huo ambao ungeweza kufanikisha makubaliano ya kumaliza mgogoro.
Kagame na Tshisekedi walikutana mara ya mwisho Oktoba jijini Paris lakini hawakuzungumza moja kwa moja, huku mazungumzo yao yakiendelea kupitia upatanishi wa Luanda.