Mwanafunzi wa Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (DIT) ameripotiwa kujirusha jana usiku, majira ya saa tano, katika tukio lililowaacha wanafunzi na uongozi wa chuo wakiwa na mshangao na huzuni kubwa.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana. Hakuna uhakika kama lilisababishwa na tatizo la afya ya akili au changamoto nyinginezo binafsi.
Akizungumza leo asubuhi, mmoja wa wawakilishi wa uongozi wa chuo hicho amesema, “Kwa sasa, tumeanza mawasiliano na wazazi wa mwanafunzi husika ili kupata ufafanuzi wa kile kilichoweza kusababisha hali hii. Tunashirikiana pia na mamlaka husika kuhakikisha tunapata taarifa kamili.”
Kwa sasa, wanafunzi wa chuo hicho wamehimizwa kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea. Viongozi wa chuo wameahidi kutoa msaada wa kisaikolojia kwa wanafunzi waliokuwepo au walioshuhudia tukio hilo.
Mamlaka zinaendelea kufuatilia kwa karibu ili kupata picha kamili ya mazingira yaliyosababisha tukio hilo.
Habari zaidi zitaendelea kutolewa pindi zitakapopatikana.