Michuano ya Kombe la Dunia kwa wanaume ya 2034 itafanyika Saudi Arabia, wakati Uhispania, Ureno na Morocco watakuwa wenyeji wa pamoja wa mashindano ya 2030, Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limethibitisha.
Mechi tatu katika mashindano ya 2030 pia zitafanyika Argentina, Paraguay na Uruguay kuadhimisha miaka 100 ya mashindano hayo.
Wenyeji wa Fainali zote mbili za Kombe la Dunia walithibitishwa katika kongamano la FIFA baada ya kupiga kura.
Mataifa yote 211 wanachama wa FIFA yaliwakilishwa katika mkutano huo kwa njia ya video.