Mwanasiasa mkongwe wa Uganda Kizza Besigye na mshtakiwa mwenzake, Obeid Lutale wamefikishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Kampala, huku kukiwa na ulinzi mkali.

Wawili hao wanakabiliwa na mashtaka manne yakiwemo ya kumiliki silaha kinyume cha sheria, tuhuma ambazo wanakanusha. Leo, watafikishwa tena katika mahakama ya kijeshi.

Wakati huo huo baraza la sheria la Uganda lilikataa kutoa leseni ya muda kwa Martha Karua, waziri wa zamani wa sheria wa Kenya ambaye alikuwa anataka kuongoza timu ya mawakili wa Besigye.

Baraza hilo lilisema kuwa maombi ya Martha yana uchochezi wa kisiasa kuliko ya kitaaluma. Hata hivyo, Martha ameapa kuendelea kuhudhuria kesi ya mahakama ya Besigye akiahidi pia kuiunga mkono timu hiyo ya wanasheria kwa uwezo wowote hata kama sio kama wakili wake.

Kiongozi huyo wa upinzani alitekwanyara alipokuwa ziarani nchini Kenya mwezi uliopita alipokuwa ziarani nchini Keny ana kupelekwa kwenye gereza la kijeshi nchini Uganda. Hatua hiyo ilizua shutuma nyingi na hofu ya mabadilishano ya siri ya taarifa za kijasusi kati ya mataifa hayo mawili jirani.