Na Mwandishi wetu
WAZIRI wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba amewataka wananchi kuacha kushabikia vitendo vya uharifu na kuepuka kujichukulia Sheria mkononi kwani sio jambo nzuri.
Dk Nchemba ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam mapema leo Desemba 8, 2025 wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Amani Simbayao aliyefariki dunia kwa kushambuliwa na wananchi wenye hasira eneo la Tegeta kwa ndevu Jijini Dar es Salaam.
Marehemu Simbayao ni miongoni mwa maofisa watatu walioshambuliwa wananchi eneo la Tegeta kwa ndevu usiku wa Desemba 5,2024 ambao walizuia gari aina ya BMWx6 lililodaiwa kutokuwa ndani ya mfumo wa Mamlaka hiyo.
Dk Nchemba amesema jambo lililotokea alipaswi kutokea kwa nchi kama ya Tanzania hasa katika uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anayesimamia utawala Bora na haki za binadamu.
“Nalani vikali vitendo hivi vya uharifu na kujichukulia sheria mkononi na ni lazima hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa wote waliousika haya mambo ayawezi kukubalika katika nchi yoyote “amesema Dk Nchemba
Aidha aliiagiza kamati ya ulinzi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwafatilia wote waliousika na kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yao.
Pia aliwaomba wananchi kuicha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufanya kazi yake kwa usalama kwani wanatimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na taratibu.
Dk Nchemba alitoa rai Kwa Kamishina wa TRA pamoja na timu yake kuendelea kufanya kazi na kutorudishwa nyuma na waovu wa namna hiyo.
“Nawaomba msirudi nyuma katika jambo la kukusanya kodi ..nyinyi amtugi sheria bali mnatekeleza hivyo tekelezeni bila ya kuongeza koma na hakuna kunyoosha mkono kwa wakwepa kodi”alisisitiza Dkt Nchemba
Awali Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda amesema TRA inalaani vikali Kwa wale wote waliojichukulia Sheria mkononi kwani Marehemu Simbayao akustahili kutendewa alivyotendewa .
Amesema ya shambulio lililotokea dhidi ya watumishi TRA akiwemo Amani walikuwa majukumu yao ya kuisaidia nchi hna wananchi kwa ujumla.
“Marehemu na wezanke walikuwa wakifanya kazi za Forodha nyingi ikiwemo Udhibiti upotevu wa mapato ya nchi ikiwemo kuzuia magendo kihalali na kisheria na kikanuni na kitaratibu ya nchi”amesema
Aidha amesema TRA itaendelea kutoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara ili wajue kwamba kinachofanywa na watumishi wa Mamlaka ya TRA ni kwa ajili yao na taifa
“Tunaendelea kutoa elimu ya haki, Mamlaka, waliyonayo watumishi wakati wakitimiza wajibu wao na majukumu yao”alisisitiza
Vilevile Kamishina Mwenda amesema TRA itaangalia namna ya kumuwezesha mjane wa marehemu kwa kumuajiri katika huduma zinazotolewa na TRA sambamba na kuwakatia tawakatia bima watoto ili waendelee kutibiwa kama awali.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amesema kifo cha Mtumishi wa TRA kimefungua ukurasa mpya kwa Mkoa huo na kusisitiza kuwa ukurasa huo ni lazima ujibu na kuleta mashahidi.
“Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa
wa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya na Mamlaka ya TRA lazima tunahakikisha eneo palipotokea tukio pasafishwe naomba nisiojiwe kuhusu hilo”amesema Chalamila.