Vyombo vya habari vya Iran vimeripoti kuwa ubalozi wa Iran mjini Damascus umeshambuliwa.
Video iliyochapishwa na Shirika la Habari la Kiarabu la Al Arabiya inaonesha uharibifu wa sehemu ya nje ya jengo hilo, ikiwa ni pamoja na madirisha yaliyovunjika, na vyumba vilivyovurugwa huku karatasi zikiwa zimetawanyika kwenye sakafu.
Picha pia zinaonesha picha kubwa kwenye jengo la jenerali wa Iran Qasem Soleimani na kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah – wote wakiwa wamefariki, likiwa limeraruliwa na umati wa watu.