Na Mwamvua Mwinyi, JamhuriMedia, Mafia
Tamasha la Utalii lijulikanalo kama “Mafia Island Festival” limefunguliwa rasmi leo Desemba 6, 2024 na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Rashid Mchatta ambaye ni mgeni rasmi wa Tamasha hilo litakalodumu kwa siku tatu.
Akikabidhi zawadi kwa washindi wa mbio za marathoni, Mchatta Amewataka vijana kujitokeza kuwania fursa zinazotolewa na Serikali pamoja na kuwahimiza kushiriki katika michezo ambayo inaimarisha afya na ni fursa kwa kuwa chanzo cha ajira.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo amewapongeza washiriki wanawake walio fanikiwa kumaliza kilomita 21 na kutoa zawadi ya kiasi cha Shilingi elfu 50 ili kuwapa hamasa wanawake wengine waweze kujitokeza kushiriki katika michezo.