Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
SPIKA mstaafu Anne Makinda ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kairuki amependekeza zifanyike tafiti kujua sababu za watoto wengi wa kiume kuachwa nyuma kitaaluma na wenzao wa kike.
Aliyasema hayo jana wakati wa kongamano la sita kitaaluma lililoandaliwa na chuo hicho kujadili namna sekta ya afya inaavyoweza kufanya mabadiliko kwa huduma hizokutolewa kidijitali.
Alisema kwa siku za karibuni watoto wa kike wameonekana kuongoza kitaaaluma na kuwaacha mbali wenzao wa kiume jambo ambalo alisema jamii haipaswi kulifumbia macho na kuliona kama la kawaida.
“Hili si jambo la kawaida kabisa na tusilichukulie kirahisi lazima tutafute sababu za kwanini hawa watoto wanaanguka kitaaluma, lazima kuna sababu kwa hiyo tukifanya utaafiti tutapataa sababu na tutachukua hatua,” alisema Anne Makinda
“Ni jambo jema kuona watoto wa kike wanakuwa mbele kielimu baada ya miaka mingi ya kuwa nyuma lakini siyo lengo letu kufurahia watoto wa kiume kuachwa nyuma, tuwapongeze watoto wa kike lakini tujue tatizo ninini, tunaposema 50-50 tunamaana twende kwa usawa” alisema
Alisema hali hiyo haiko Tanzaniania pekee bali katika mataifa mbaalimbali watoto wa kiume wameanza kuachwa nyuma kimasomo na wenzao wa kike jambo ambalo alisema lisiachwe kama lilivyo na likaonekana la kawaida.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benjamin Mkapa Fundation, Dk Ellen Senkoro alisema wamejadili namna teknolojia inavyoweza kurahisisha utoaji wa huduma za afya na kufuatilia hali za wagonjwa.
“Tumesikiliza bunifu mbalimbali za wahitimu wa chuo hiki na wale waliohitimu miaka ya karibuni kwa kweli bunifu zinavutia sana na kazi ambazo wanafanya kidijitali zinatia moyo kwa hiyo nawahimiza madaktari wataohitimu wawe wabunifu huduma hizi zitolewe kidijitali,” alisema
Dk. Ellen alisema kwa kuwa umeme siyo tatizo tena nchini ni rahisi madaktari hao wakabuni mifumo ambayo wataitumia kuhudumia wagonjwa wao kwani watanzania wengi wanasimu janja.
“Mabadiliko duniani yanakwenda kwa kasi kwa hiyo lazima tuwe wabunifu ifikie wakati siyo lazima sana kwenda hospitali au kituo cha afya, unaweza ukafanya vipimo ukiwa nyumbani na ukapata majibu yako kwa kutumia simu yako ya mkononi,” alisema
Alisema amefurahishwa kuona tuzo nyingi zilizotolewa kwenye kongamano hilo zimechukuliwa na wahitimu wa kike na kwamba halihiyo inaonyesha kuwa kuanzia mfumo wa sekondari wanafunzi hao wameandaliwa vizuri.
“Mafanikio haya yanaonyesha kuwa wanawake tunaweza kushika nafasi mbalimbali za uongozi tofauti na mitazamo ilivyokuwa zamani na hivi sasa tuna kazi kubwa ya kuhakikisha tunawawezesha watoto wa kiume kujua kwanini wanarudi nyuma ili tuweke uwiano,” alisema
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Kairuki, Profesa Yohana Mashalla, alisema kongamano hilo la mwaka huu lilikuwa mahsusi kwa ajili ya kujadili matumizi ya dijitali katika kufanikisha utoaji wa huduma za afya kwa urahisi nchini.
“Tumejiuliza dijitali ipo watumiaji wapo, je gharama zake zikoje na halafu kwa sababu ziko nyingi ni ipi gharama yake tunaweza kuimudu kuinunua kwa mazingira ya hapa nchini,” alisema Prof Mashalla.
“Hizi teknolojia zinakuja na zinabadilika mara kwa mara tunapaswa kujiuliza je tuna wataalamu au vyuo vya kutosha vitakavyofundisha namna ya kutumia teknolojia hizo na zinavyotumika kwa usahihi,” alisema.