Na Magrethy Katengu,JamhuriMedia,
Dar es salaam

Serikali imesema itaendelea inahakikisha inaweka mikakati madhubuti ya kuwawezesha watanzania zaidi ya 1000 kupata fursa ya ajira nje ya nchi

Akizungumza jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2024 Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi,Ajira na wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete katika hafla ya kuwaaga wauguzi waliopata fursa ya kupata za kazi kwenda nchi Saud Arabia amesema huo mwanzo mzuri wa Mashirikiano.yaliyoanzishwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassani.

“Tukio hili ni la kipekee ambalo Rais Dkt Samia alianzisha Diplomasia ya Uchumi na itakumbukwa Novemba 2023 mlishuhudia kuwekeana saini ya hati mbili za mashirikiano kati ya Nch yetu na serikali ya Saud Arabia kuhusu utaratibu wa ajira na makubaliano hayo yalitoa fursa kwa watanzania 500 waweze kuajiriwa Saud Arabia huvyo mpaka sas zaidi ya watanzania zaidi ya 240 wameshapata ajira huko”amesema Waziri

Waziri amewashauri hao wote waliopata fursa za ajira katika nchi hiyo kwenda kufanya kazi kwa bidii kuwa waadilifu ili waendelee kuaminiwa na kulitangaza taifa lao vizuri huku wengine wakiendelea kufanyiwa mchakato wasikataliwe kupitia hao waliotangulia .

Serikali imeweka malengo mahususi ya kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania kutoka 556,065 kwa mwaka 2022 hadi 1,000,000 ifikapo mwaka 2028,” amesema

Waziri Ridhiwani Kikwete, amebainisha kuwa Serikali imesaini makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya ajira na nchi ya Falme za Kiarabu (UAE), Saudi Arabia, Iran na Qatar kwa lengo la kuongeza fursa zaajira kwa watanzania kwenye nchi hizo.

Aidha, Mhe. Ridhiwani amesema serikali inatekeleza mpango wa kuwaandaa vijana kuwa na ujuzi stahiki unao wawezesha kumudu ushindani kwenye soko la ajira la kimataifa sambamba na kufanya kazi zenye tija.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Diasapora na fursa cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Salvator Mbilinyi Sambamba na hayo, ametoa rai kwa wauguzi wanao kwenda kufanya kazi nchini Saudi Arabia, kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ili kuaminika na kuiletea heshima nchi yao Tanzania.