Israel iliitaarifu Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) Jumatano hii, Novemba 27, kuhusu nia yake ya kukata rufaa dhidi ya hati za kukamatwa zinazomlenga Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na Waziri wake wa zamani wa Ulinzi Yoav Gallant kwa uhalifu wa kivita, ofisi ya Benjamin Netanyahu imetangaza.
Ikisubiri uamuzi kwa undani, Israel pia imeitaka ICC kusitisha utekelezaji wa hati hizi mbili za kukamatwa, ofisi ya Waziri Mkuu wa Israeli imesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Uamuzi huu wa chombo cha mahakama kilichoko The Hague uliibua hisia tofauti kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, hata miongoni mwa nchi 125 zilizoidhinisha Mkataba wa Roma ulioanzisha ICC.