Maafisa wa uokoaji waliyapata mabaki ya ndege kwenye eneo la milima lakini ilichukua saa kadhaa kwa timu kufika eneo la ajali. Shirika la Msalaba Mwekundu liliripoti Jumanne aliyenusurika alikuwa amepelekwa hospitali.

Shirika la msalaba mwekundu limesema watu watano wamekufa baada ya ndege ndogo chapa Cessna 206 Stationair iliyokuwa imebeba watu sita kuanguka katika eneo la kusini mashariki mwa mji mkuu wa Costa Rica, San Jose.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 31 aliyenusurika katika ajali hiyo yuko katika hali mahututi.

Ndege hiyo ilianguka siku ya Jumatatu karibu na mlima wa Pico Blanco muda mfupi baada ya saa sita mchana wakati ilipopoteza mawasiliano na kutoweka kwenye mtambo wa rada.

Ndege hiyo ilikuwa njiani kuelekea San Jose ikitokea pwani ya kaskazini ya Costa Rica. Chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa.