Ayatollah Ali Khamenei, Kiongozi wa Iran katika hotuba yake katika kikao na “Wanajeshi wa nchi nzima” alisema “Waranti ya kukamatwa kwa Netanyahu kwa uhalifu wa kivita haitoshi, ni lazima hukumu yake ya kifo itolewe.”

Pia alisema: “Adui hajashinda huko Gaza na Lebanon, huu ni uhalifu wa kivita.” Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) hivi karibuni ilitoa hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyau.

Wapumbavu wasifikiri kwamba walishinda kwa sababu walipiga mabomu nyumba, hospitali na mikusanyiko.” “Hakuna anayezingatia haya kuwa ushindi.”

Katika hotuba ya leo, Hossein Salami, kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na Ismail Qaani, kamanda wa Kikosi cha Quds walihudhuria.

Ayatollah Khamenei kwa mara nyingine tena aliahidi katika hotuba hii kwamba “utawala wa Kizayuni bila shaka utaangamizwa.”

Mamlaka za Iran haziitambui Israel na kuitaja kuwa ni “utawala wa Kizayuni”. Katika miezi iliyopita, migogoro ya moja kwa moja ya kijeshi kati ya Iran na Israel imefikia kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.

Baada ya Israel kushambulia maeneo kadhaa ya kijeshi nchini Iran tarehe 5 Novemba, uvumi mwingi umeibuliwa kwenye vyombo vya habari na duru za kidiplomasia kuhusu lini na jinsi gani Iran inaweza kujibu.

Katikati ya mwezi wa Novemba, Bw. Khamenei, katika hotuba yake ya hadhara katika mkesha wa kuadhimisha miaka 45 ya kutekwa nyara katika ubalozi wa Marekani mjini Tehran, alisema kuhusu makabiliano ya kijeshi na Israel na Marekani kwamba maadui watapata ” majibu ya makali”.