Huku hatua ya mwanasheria Jack Smith ya kufuta mashtaka ya kuingilia uchaguzi wa 2020 dhidi ya Donald Trump, moja ya vitisho vya mwisho vya kisheria vilivyosalia dhidi ya rais mteule imegeuka kuwa majivu na kupeperushwa na upepo.

Smith pia anatupilia mbali rufaa ya kesi dhidi ya Trump kwa kutumia vibaya hati nyeti za usalama wa kitaifa baada ya kuondoka Ikulu ya White House mnamo 2021.

Hizo zilikuwa kesi mbili kubwa zaidi dhidi ya Trump, ambazo zilikuwa zikimkabili kwa zaidi ya mwaka mmoja alipoanza mbio zake za kurejea Ikulu ya White House.

Ushindi wake mnamo Novemba na matarajio kwamba atamaliza kile alichokiita “utekaji nyara wa kisiasa” wa mfumo wa kisheria baada ya kuchukua madaraka mnamo Januari, ulibadili upepo kutokana na tangazo la Jumatatu la Smith.

Mwongozo wa Wizara ya Sheria unakataza mashtaka ya jinai kwa rais aliye madarakani. Katika jalada lake, Smith alisema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ilihitimisha hivi karibuni kwamba ulinzi huu wa kisheria pia unatumika kwa mashtaka ya raia binafsi ambaye anachaguliwa kuwa rais baadaye.