Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Tanga

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imeibuka kidedea baada ya imefanikiwa kunyakuwa Ubingwa wa Jumla wa Mashindano ya SHIMMUTA kwa mwaka 2024 katika michuano iliyofanyika jijini Tanga.

Katika mashindano hayo ambayo yalifungwa rasmi na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo, yalishuhudia timu nne za TPA zikitawazwa mabingwa rasmi wa mashindano hayo.

Timu ya kwanza kutwaa ubingwa wa mashindano hayo, ni timu ya mpira wa kikapu ya TPA ambayo iliichabanga timu ya NSSF kwa jumla ya vikapu 57 – 45 katika mchezo wake wa fainali. Ubingwa huo ni wan ne mfululizo kwa kwa timu hiyo ya TPA.

Katika mchezo wa mpira wa pete “Netball” timu ya TPA ilitwaa ubingwa huo kwa kuifunga timu ya TMDA kwa magoli 53 – 43 katika mchezo wa fainali ya mashindano hayo. Huo ukiwa ni ushindi wanne mfululizo kwa timu hiyo ya TPA kutawazwa mabingwa wa mashindano hayo kwa mchezo huo.

Kwa upande wa mpira wa Kamba, timu ya wanawake na wanaume zote za TPA, zilishinda michezo yao ya fainali, ambapo timu ya wanawake iliikung’uta timu TPDC, huku wanaume wakiigalagaza timu ya TBS kwa kuichapa katika mtanange uliozikutanisha timu hizo. Timu zote mbili za TPA zimetwaa ubingwa huo kwa mara ya tatu mfululizo.

Na kwa upande wa mchezo wa riadha, timu ya TPA ilishinda katika mbio za mita 200 na kujinyakulia medali za dhahabu, huku katika mikimbio ya wazee ya mita 100, timu ya TPA iliibuka kidedea kwa kupata ushindi wa pili na kujinyakulia medali ya fedha.

Katika michezo ya jadi, timu ya TPA haikuondoka mikono mitupu kwani mwanamama Celine Simon alionyesha umahili wake kwa kuibika mshindi wa tatu katika mchezo huo wa kusogeza kete yaani ‘draft’.

Kufuatia ubingwa huo wa timu zake, TPA imeibuka mshindi wa jumla kwa mara ya pili mfululizo. Mara ya kwanza kuwa mshindi wa jumla ni mashindano ya mwaka 2023 yaliyofanyika mjini Dodoma. Katika mashindano yaliyofanyika mjini tanga mwaka 2024, jumla ya timu.