Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Tanga

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania imefanikiwa kuingiza timu nne katika fainali ya mashindano ya SHIMMUTA yanayoendelea jijini Tanga.

Timu ya Netball imeingia fainali baada ya kuifunga TRA jumla ya magoli 48 – 43 katika mchezo wa nusu fainali iliyochezwa katika viwanja vya Harbours Club.

Kwa upande wa timu ya mpira wa kikapu imeingia hatua ya fainali baada ya kuifunga TRA jumla ya vikapu 42 – 24

Timu za Kamba wanaume na wanawake zote zimeingia fainali,wanaume watacheza fainali na timu ya TBS wakati ile ya wanawake itacheza na TPDC.

Na timu ya mpira wa wavu ( Volleyball) wanawake wamefanikiwa kunyakuwa ushindi wa tatu wa michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa set 3 -1 dhidi ya DUCE.

Upande wa riadha mita 200 Shaggy Lugua ameshinda na kujihakikishia medali ya dhahabu wakati kwa mbio za mita 100 za wazee,Hassan Ahmed ameibuka mshindi wa pili,katika michezo ya jadi upande wa ‘draft’ Celine Simon amejihakikishia nafasi ya mshindi wa tatu.