Balozi Mteule wa Korea Kusini nchini Tanzania Eunju Ahn amekutana na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar na kueleza kufurahishwa kwake juu ya utendaji wa Jeshi la Polisi Tanzania kwa kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama kwa wageni na watalii wanaofika Zanzibar.

Akizungumza na Maafisa hao Makao Makuu ya Polisi Zanzibar Balozi Eunju ameeleza kuwa, Korea Kusini itaendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kwa Tanzania na kutoa fursa mbalimbali kwa Jeshi la Polisi ikiwemo mafunzo ili kuwajengea uwezo na kubadilishana uzoefu baina ya pande hizo mbili.

Nae Naibu Mkurugenzi wa Upeleezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Zuberi Chembera kwa niaba ya kamishna wa Polisi Zanzibar amesma kuwa, Jeshi la Polisi linatambua umuhimu wa shughuli za utalii, hivyo litaendelea kuimarisha usalama uliopo nchini kwa raia na wageni wote wanaofika Zanzibar.