Na Isri Mohamed
Klabu ya Simba leo Novemba 20, 2024 imezindua rasmi jezi mpya watakazotumia kwenye mashindano ya kimataifa wanayoshiriki ambayo ni kombe la shirikisho barani Afrika ( CAFCC)
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jezi hizo iliyofanyika Katika duka la Sandaland kinondoni, Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu amewataka mashabiki kuzichangamkia jezi hizo mapema.
“Kipekee tunamshukuru Sandaland kwa utekelezaji wa haya mambo, jezi ni nzuri n naamini Wanasimba watajitokeza kununua kwa wingi”
Nae Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally ametoa taarifa ya kikosi baada ya kumalizika kwa Mechi za kimataifa ambapo wachezaji wao kadhaa walikwenda kushiriki.
“Kikosi kwa sasa kinaendelea na programu ya mazoezi kikijiandaa na mchezo dhidi ya Pamba, leo usiku tutaondoka kwenda Mwanza, na wachezaji wanne waliokuwa Taifa Stars na Camara aliyekuwa timu ya Taifa ya Guinea ameshajiunga na kambi, Steven Mukwala atawasili Dar kesho asubuhi na kuunganisha kuja Mwanza”
Simba watazitumia jezi hizo mpya kwa mara ya kwanza kwenye mechi yao ya Kombe la shirikisho hatua ya makundi dhidi ya FC Bravos itakayochezwa Novemba 27, katika dimba la Benjamin Mkapa.