Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Songwe
Mahakama ya Wilaya ya Songwe imemhukumu Bw. Assan Jacob Kalinga aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Mbuyuni H/W ya Songwe, adhabu ya kwenda Jela miaka Ishirini (20).
Adhabu hiyo imetolewa kwa Kosa la ufujaji na ubadhirifu K/f cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura 329 Mapitio ya Mwaka 2022 ikisomwa pamoja na Aya ya 21 ya Jedwali la kwanza na Kifungu cha 57(1) na 60(2) cha Sheria ya Udhibiti wa Makosa ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupangwa sura ya 200 Mapitio ya Mwaka 2022.
Hukumu dhidi ya Assan Jacob Kalinga imetolewa Katika Kesi ya Uhujumu Uchumi namba 10/2023, Novemba 18, 2024 Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mh. A. Lugome.
Kesi hiyo imeendeshwa na Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU Bi Simona Mapunda.
Imeelezwa kuwa Mshtakiwa alifikishwa Mahakamani baada ya kufanya ubadhirifu wa fedha kiasi cha Tsh. 7,721,000/- Mali ya Wanakijiji cha Mbuyuni walizochanga kulipia mita za Umeme wa REA kati ya mwezi April 2020 Hadi oktoba 2020.
Mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha Miaka 20 Jela