Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime amesema “Tunasisitiza Wanahabari wapewe mafunzo ya Usalama, mfano ukiona mahali unaenda kuripoti unatakiwa kujua usimame upande gani, usisimame wapi.”

Amesisitiza “Kusimama upande ambao unataka uone bomu la machozi linavyotoka ili upate picha nzuri sio sawa, unaweza kupata madhara na linaweza kukumaliza wewe, ukiambiwa unasema ‘Wananchi wana haki ya kupata taarifa sahihi’, singatia usalama wako kwanza.”

Aidha, amewataka Wanahabari kuwa na wajibu wa kutoa elimu kuhusu Haki na wajibu wa Mpiga Kura.