Na Haji Mtumwa, JamhuriMedia, Zanzibar

Jamii visiwani humu imeaswa kutumia vyoo vya kisasa katika maeneo ya makaazi, Shule na sehemu za kijamii Ili kujikingaa na maradhi yanayoweza kuepukika.

Akizungumza mara baada ya kutoa elimu hiyo ya matumizi ya vyoo vya kisasa, katika maadhimisho ya matumizi ya vyoo kwa wanafunzi wa Shule ya Michakaeni kisiwani Pemba.

Kiongozi wa timu ya madaktari wa kichina, Dr Dai Yangi alisema Kuna umuhimu mkubwa kwa Jamii kutumia vyoo vya kisasa Ili kuendana sambamba na mabadiliko ya midunia.

Alisema matumizi ya vyoo vya kisasa vina nafasi kubwa ya kuifanya Jamii kuepukana na maradhi mbali mbali yakiwamo ya kuambuliza, jambo ambalo linahitaji kuungwa mkono Kwa Kila mwana Jamii.

“Utumiaji wa vyoo vya kisasa linamgusa kila mwananchi hivyo ni lazima kulipa uhumu suala hilo kwani linasaidia sana hasa kwa kujikinga na maradhi ya miripuko pamoja na ugonjwa wa kichocho” alisema.

Mratibu wa kitengo cha Maradhi yasiyopewa kipaumbelea Dr. Saleh Juma Muhammed alisema kupitia maadhimisho hayo wametoa elimu kwa wanafunzi ili wapate uwelewa wa matumizi bora ya vyoo pamoja na kuyatambua maradhi ya ugonjwa wa kichocho na athari zake.

Alifahamisha kuwa katika kuhakikisha wanaondosha ugonjwa wa kichocho jitihada zainafanyika kwa kutoa elimu ya afya kwa wananchi ili kufahamu madhara yatokanayo na ugonjwa huo .

Sambamba na hayo alisema kwamba kitengo cha Maradhi yasiyopewa kipaumbele kinaendelea kutibu maji katika mito na maziwa kwa kutia dawa ili kuuwa konokono ambao wanaishi katika mito na kuzalisha wadudu wa kichocho .

Nae Dr Hu Wenjun kutoka kitengo cha Maradhi yasiyopewa kipaumbele Zanzibar amesema tatizo la ugonjwa wa kichocho bado lipo na linawaathiri wananchi walio wengi hivyo, kupita elimu waliyopatiwa wa wanafunzi hao itawasaidia kujikinga na maradhi ya ugonjwa wa kichocho.

Hata hivyo aliwataka wanafunzi hao kuwacha tabia ya kuoga katika mito na maziwa ili kuepusha kupata mambukizi ya ugonjwa wa kichcocho unawoweza kuwaathri na kushindwa hata kuendelea na masomo yao kwa ufanisi .

Aisha Sharifu Ali wanafunzi wa skuli ya Michakaini alisema kupitia mafunzo waliyoyapata yataweza kuwasaidia kujikina na ugonjwa huo .

Mundhiri Abdalla Shaibu Mwanafunzi wa skuli hiyo ya Michakaini Msingi akitaja dalili za ugonjwa wakichocho alisema ni kupanuka kwa kibofu cha mkojo mkuvimba kwa ini ,kukojoa damu wakati wa kujisaidia kupata muwashao na vidonda na kuwataka wanafunzi wenzake kuchana kabisa na vianzio vinavyo changia upatikanaji wa maradhi ya kichocho .