Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanya Mkutano wa Pembezoni mwa Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) mjini Baku, Azerbaijan, ukiwa na agenda inayohusu Uvuvi Endelevu na Uchumi wa Buluu. Lengo la Mkutano huo ni kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji katika Sekta ya Uvuvi na juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Mkutano huo ulifunguliwa na kuogozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ambaye aliwakilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muunganonnw Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji leo Novemba 14, 2024