Na Magrethy Katengu,JamuhuriMedia, Dar es Salaam
Jumuiya ya la Waandishi wa Mtandaoni Tanzania (JUMIKITA) wameshauriwa kuzingatia weledi ,maadili, katika kuandika habari kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji ili kusaidia kutoa taarifa za uhakika na zenye ukweli kwa wananchi kuepuka kuleta taharuki ndani ya Jamii.
Rai hiyo imetolewa leo Novemba 13, 2024 jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Tamisemi Dkt Grace Maghembe wakati akifungua semina ya siku moja JUMIKITA kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivyo ni vyema waandishi kutumia kalamu zao vizuri wanaporipoti taarifa za uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu .
” Tumeamua kutoa mafunzo haya yanayoendana na tukio kubwa la ambalo wananchi wanaokwenda kufanya maamuzi nani awaongoze Kwa miaka mitano na lengo la Serikali ni kuona uchaguzi huo unakua huru na haki, hivyo ni vyema kwa waandishi wa habari kuandika habari zenye ukweli ili kuweka utulivu na amani ndani ya nchi” amesema Dr Magembe
Sanjari n hayo , amewashauri wananchi kuwapima viongozi wanaowachagua kwa hoja zenye maslahi mapana ya nchini na sio kuchagua viongozi ambao hawawezi kuwajibika kuwaletea maendeo ndani ya mitaa yao.
Dr Magembe ameshauri Mamlaka taasisi za Serikali kutambua umuhimu wa waandishi wa habari wanapokua kwenye majukumu yao kwa kuwapatia vitambulisho maalumu ili kuepuka changamoto ambazo zinakua zinajitokeza ikiwemo vurugu.
Naye, Afisa Sheria wa Tamisemi Mihayo Kidete amesema kanuni ya Tanzania ili mtu aweze kupata nafasi ya kugombea nafasi yoyote ni lazima awe kuanzia umri wa miaka 21 na awe amejindikisha katika daftari la mpiga kura na kutimiza masharti yote yaliowekwa katika kanuni za uchaguzi.
“Mtu hatakua na sifa za kugombea nafasi yoyote katika uchaguzi endapo ataajiriwa au kuteuliwa katika wadhifu wowote katika utumishi wa umma au kuchaguliwa katika nafasi ya udiwani, ubunge, uspika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania umakamu wa Rais au Rais wa nchi”amesema Mihayo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumikita Shaban Matwebe ameshukuru na ameipongeza Ofisi ya Rais tawala za Mikoa Tamisemi kwa kuona umuhimu wa kuwapa elimu wanahabari za mtandaoni kwani ulimwengu wa sasa ni wakidigital wanaofitiliwa sanaa poote mtu alio kupitia simu anajua nini kinaendelea.
Matwebe amesema wanamitandao ya Kijamii ni wanahabari, ambao wanatembea na vifaa vyao mkononi hufanya kazi popote walipo hivyo amewahakikishia Tamisemi baada ya semina hiyo wataona mabadiliko makubwa taarifa zenye weledi na wananchi watajua kanuni za uchaguzi .