RAIS mteule wa Marekani Donald Trump amemteua Susie Wiles kuwa afisa mkuu wa utumishi wa ikulu ya White House. Huo ni uteuzi wa kwanza wa Trump baada ya ushindi wake kwenye uchaguzi wa Novemba 05 dhidi ya Kamala Harris.

Kupitia taarifa, Rais mteule wa Marekani Donald Trump alimteua meneja wake wa kampeni, Susie Wiles, kuwa mkuu wa wafanyakazi wa Ikulu ya White House. Huo ukiwa uteuzi wake mkuu wa kwanza tangu kushinda uchaguzi wa wiki hii.

Trump alimmiminia sifa Susie akisema “Susie ni imara, mwerevu, mbunifu, anapendwa na kuheshimiwa kote”. Aliongeza kuwa “Susie ataendelea kufanya kazi bila kuchoka ili Kuifanya Amerika iwe bora zaidi tena. Ni heshima inayostahiki kuwa na Susie kama Mkuu wa kwanza mwanamke wa utumishi wa White House katika historia ya Marekani.”

Siku mbili tu baada ya uchaguzi mkuu, na miezi miwili na nusu tu kabla aingie ikulu, ushindi wa kishindo wa Donald Trumpdhidi ya Mdemocrat Kamala Harris tayari unatikisa siasa za Marekani na ulimwengu.