Watu zaidi ya 17 wameuawa katika mlipuko kwenye kituo cha treni katika wilaya Balochistan nchini Pakistan wakiwemo wanajeshi 14 , mamia ya wengine wakiripotiwa kujeruhiwa kwa mujibu wa taarifa ya polisi.

Mamlaka imeliambia Shirika la Habari la AFP kwamba huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka wakati huu waliojeruhiwa wakiendelea kupokea matibabu.

Mlipuko umetokea wakati abiria wakisubiria usafiri wao katika mji wa mkuu wa wilaya ya Balochistan, eneo jirani na mataifa ya Afghanistan na Iran.

Wilaya ya Balochistan na yenye idadi kubwa ya watu nchini Pakistan inakaliwa na makundi ya watu wanaotaka kujitenga, wilaya hiyo pia ikiwa na utajiri wa rasilimali.

Watu wenye silaha wamekuwa wakiripotiwa kutekeleza mashambulio dhidi ya miradi ya nishati ambayo inafadhiliwa na mataifa ya kigeni haswa kutoka nchini China.

Makundi hayo yenye silaha yanawatuhumu raia wa mataifa ya kigeni kwa kuwatenga wenyeji katika faida wanayoipata kutokana na shughuli zao kwenye ardhi yao.

Baloch Liberation Army (BLA) mojawapo ya makundi yenye silaha yamekiri kuhusika na mashambulio mabaya dhidi ya maofisa wa usalama au hata raia wa Pakitsan kutoka katika majimbo mengine haswa Punjabi.

Mwezi Agosti, kundi hilo lilikiri kuhusika na kupanga mashambulio ya waasi yaliosababisha karibia vifo vya watu 39 mojawapo ya idadi kubwa ya watu kuuawa na waasi katika eneo hilo.