Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Wahariri na Waandishi wa habari nchini,wametakiwa kuweka maazimio machache yatakayokwenda kufanyiwa kazi kama sehemu ya kukuza taaluma ya habari eneo la weledi.
Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Katibu mkuu Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari , Nicholaus Mkapa alipokuwa mgeni rasmi akimwakilisha waziri mwenye dhamana , kwenye mkutano wa Nane wa Jukwaa la Wahariri TEF.
Mkapa amesema maazimio watakayo watoa ,yalenge, kujibu lila mlichokieleza, ili kuhimiza vyombo vya habari kufanya kazi kwa kuzingatia weledi wa taaluma sheria na maadili mwishowe kujenga uaminifu mbele ya umma tunaoutumikia
“Mnapokuwa na lengo la kuwa na vyombo vya habari,vinavyoaminika mbele ya umma kuna umuhimu wa kuwa na mkakati wa kuwezesha tasnia ya habari kufikia viwango” amesema.
Amesema kwa sasa, Wizara imeendelea kufanya mapitio ya sera ili kuweka mwelekeo mzuri hasa kipindi hiki ambacho matumizi ya TEHAMA ni makubwa na vyanzo muhimu katika kifikisha habari .
Pia mifumo ya kisheria imeendelea, kuboreshwa na imeleta mafanikio makubwa katika sekta ya habari ikiwemo uwanzishwaji wa bodi ambayo ina sura ya wanahabari
Amesema Wizara bado inaendelea kufanyia kazi maekezo ya makampuni ambayo yanadai Serikali yawasilishe nyaraka ili kurahisisha maelekezo Kwa muda kuhusu kumiliki asilimia 51 kwa wenyeji na 49 Kwa wenyeji hili ni suala la kisera linalohitaji marekebisho kwanza ya kisera na mchakato
Kama Serikali tunasikia fahari kuona tunafanya kazi pamoja na kuwa sehemu kudumisha amani na utulivu na hivyo kuupeleka taarifa sahihi Kwa wananchi na kuwa kichocheo cha maendeleo
Mkapa amesema kipindi hiki muhimu kwa vyombo vya habari,hasa tunapo elekea kwenye uchaguzi kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia Sheria na miongozo iliyopo inayoongoza sekta hii.
“Wahariri mnatakiwa kufanya kazi yenu ya gate keeper kipindi hiki, Kwani Kuna habari nyingi za upotoshaji na zinachagizwa na ukuaji wa kitechnolojia ya habari ambapo Kuna mitandao ya kijamii ambayo imekuwa na nguvu na ushawishi katika kutoa habari
hivyo natoa wito kwa wale wenye vyombo vya habari visivyo na mfumo wa kiusanifu kuhakikisha wanasimamia na kufanya kazi zao Kwa weledi huku wakizingatia maadili ya kazi zao” amesema.
Amesema mafunzo waliyoahidi kutoa kwa Waandishi wa habai vijana ,yatasadia utoaji wa habari sahihi zilizokidhi vigezo vya habari zinazo zingatia weledi na msingi ya utaoji habari .
Amedai Wahariri na Waandishi wanao wajibu wa kudumisha umoja ,amani mshikamano kupitia kalamu na sauti zao ili kuhakikisha nchi inapiga hatua za kimaendeleo.
Pia ni muhimu kuijulisha dunia na Watanzania juu ya miradi mbalimbali iliyofanywa na Serikali nchini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa Wilaya Ilala Edward Mpogoro amesema wanahabari wanamchango mkubwa kwa Serikali ,wilaya na mkoa kwa sababu fedha nyingi ambazo Rais Samia Suluhu Hassan anazipeleka maeneo mbalimbali taarifa zisingeweza kuwafikia Watanzania na Duniani kama vyombo. vya habari visingeunga mkono kwa kila hatua.
Mpogolo ametoa wito wa vyombo vya habari kuendelea kushirikiana na Serikali na wilaya hasa pale wanapotaka ufafanuzi wa jambo
Wito wangu kwenu naombeni mzingatie suala zima la kuhubiri amani, upendo na maadili kwa jamii
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri TEF Deodatus Balile, amempongeza msajili wa hazina kwa kuanzisha utaratibu mzuri wa viongozi wa Taasisi za umma kuongea na Wahariri na Waandishi kupata fursa ya kuuliza mbalimbali na kuwezesha kuongeza nafasi ya kuaminiana japo wapo wachache kwa sasa ambao bado ukiwaendea hawataki kutoa ushirikiano wakiamini wasipotupa ushirikiano hatuwezi kutoa taarifa, sasa tunaomba utupelekee salamu zetu hata wasipotoa ushirikiano habari haifi kwakua chanzo tu cha habari ni cha uhakika.
Pia tunaomba uwahamasishe ,Mawaziri wawe na utaratibu wa kuzungumza na vyombo vya habari aidha jukwaa hilo limeelezea kusikitiahwa kwake na mwenendo wa waziri mwenye dhamana Jerry Slaa Kwa tabia yake ya kutohidhulia matukio muhimu ya kihabari.
Balile amesema Jukwaa hilo lilianzishwa mwaka 2009 likiwa na lengo kuu la kusimamia taaluma ya habari ,uhuru wa kutoa maoni uhimilivu wa kiuchumi Kwa vyombo vya habari na kukuza weledi wa kitaaluma
*Msingi wa Jukwaa unategemea katika sauti ya wasio na sauti ,Kwa kuchunguza na kuhabarisha umma iwapo Taasisi za umma zinatenda.