Na Lookman Miraji

Kwa mara nchini maonyesho ya bidhaa za vifungashio vya makaratasi yamezinduliwa jijini Dar es Salaam, hapo jana.

Maonyesho hayo yajulikanayo kama “Pro paper Tanzania” yamejumuisha kampuni mbalimbali za utengenezaji wa vifaa vya upakiaji kutoka nchi mbalimbali.

Pazia la msimu huu wa kwanza wa maonyesho hayo yalifunguliwa rasmi na naibu balozi wa India nchini Manoj Verma alisema kuwa amefurahia kuwa mgeni rasmi katika maonyesho hayo huku akifurahishwa kuona idadi kubwa ya kampuni kutoka nchini India zikishiriki maonesho hayo.

“Najisikia furaha sana kushiriki katika maonesho haya kwa mwaka huu, na nina furaha zaidi kuona idadi kubwa ya kampuni kutoka nchini India zikishiriki katika kuonyesha bidhaa zao kwani zitaweza kupanga vipaumbele hapa Tanzania ili kuwa viwanda endelevu vya makaratasi na najua kuwa matumizi ya plastiki yamekithiri Tanzania hivyo matumizi ya karatasi ni mpango sahihi kwa wakati ujao”.

Kwa upande wa waandaji wa maonesho hayo hayo kupitia Mkurugenzi mtendaji wa maonesho hayo Bwn: Jeen Joshua amesema kuwa maonesho hayo yamekuja wakati sahihi ambapo dunia ipo katika jitihada za kuhama kutoka katika matumizi ya plastiki kwenda kwenye matumizi ya marakatasi hivyo maonesho hayo yamekuwa ni mojawapo ya sehemu ya kuunga mkono jitihada za kuunga mkono serikali katika kufikia malengo yake kama taifa.

“Sote tunatambua kuwa dunia nzima iko katika mchakato wa kuhama kutoka katika matumizi ya plastiki kwenda katika matumizi ya karatasi hivyo hilo ni zoezi endelevu lililowekwa na kila serikali kuona wanafanikiwa katika mageuzi hayo.”

Aidha pia Mkurugenzi huyo wa ametoa wito kwa makampuni na wadau wanaojishughulisha katika sekta hiyo ya biashara kuweza kujitokeza katika maonesho hayo na kujionea teknolojia mpya zitumiwazo na kampuni mbalimbali kutoka katika nchi zilizoendelea.

Maonesho yataendelea kwa siku mbili mpaka kufikia novemba 9 yatakapokamilizika.