Jukwaa Wahariri Tanzania (TEF), limesikitishwa wa mwenendo wa Waziri wa Habari, Jerry Sila kutohudhuria matukio muhimu ya kihabari anayoalikuwa kama mgeni rasmi.
Hayo yamebainika leo katika mkutano TEF ulioanza jijini Dar es Saalam ambapo alikuwa mgeni rasmi na badala yake akamtuma
mwakilishi.
Mwenyekiti TEF, Deodatus Balile amesema anasikitishwa na mwenendo huo ambapo awali alialikwa katika Tuzo za Umahiri Uandishi wa Habari (EJAT), zilizotolewa Septemba 28. 2024 lakini hakufika.
Mkutano huo umeanza leo Novemba 7 na unatarajia kumalizika Novemba 9 wenye kauli mbiu ‘ Weledi kwa Uhimilivu wa Vyombo vya Habari’